Bongo News

Mgogoro wa Star Tv na Startimes


 Kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki Kituo cha Televisheni cha Star, iko katika mgogoro na Kampuni ya Ving’amuzi ya Startimes na kufikia uamuzi wa kuitoa kurusha matangazo ya televisheni ya kituo hicho.
Hatua hiyo ya Kampuni ya Startimes kuondoa Star Tv kwenye orodha ya vituo vinavyopatikana kwenye king’amuzi chake ilianza juzi.
Startimes ilianza kutoa taarifa kuwa kutokana na matakwa ya Star Tv, wameamua kuitoa kwenye orodha ya chaneli zao bila ya ufafanuzi wa kina kuhusu uamuzi huo.
Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, alipotafutwa kutolea ufafanuzi wa kitendo hicho, alisema hafahamu lolote.
“Sifahamu kwani niko Pemba lakini labda watafute Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (Mkurugenzi wa TCRA) watakuwa wanajua,” alisema Profesa Mbarawa.
Profesa Nkoma hakupatikana jana na juhudi za gazeti hili zilifanikiwa kumpata Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi aliyesema hafahamu sababu za Startimes kuitoa Star Tv katika kurusha matangazo ya dijitali.
“Kulikuwa na matatizo ya makubaliano baina ya pande hizo mbili, Star Tv walilalamika jinsi ya kuonekana kwa chaneli yao kwa mtoa huduma,” alisema Mungi.
 Mungi alisema kwa mujibu wa leseni ya kurusha matangazo ya kimataifa, Star Tv inatakiwa kuonekana katika dijitali zote za ndani na uamuzi waliochukua unakiuka makubaliano hayo. “Hata kama kulikuwa na matatizo, hawakutakiwa kuchukua uamuzi huo, kwani wangekutana na mamlaka husika (TCRA) na kusikiliza malalamiko hayo kisha kuwasuluhisha na tatizo hilo likamaliza,” alisema Mungi.

3 comments:

abuy_ally said...

ONGERA KAKA KWA POST NZURI

mybusinessmanual.blogspot.com said...

asante Brother ,tuendelee kuwa pamoja katika kujenga nchi yetu yenye rasilimali nyingi lakini zinatumiwa vibaya

mybusinessmanual.blogspot.com said...

asante kaka