Wednesday, September 26, 2012

No Financial Benefit in Freemason says Sir Chande

     

  There is No financial benefits in freemasonry , huu ni msemo ambao Sir Jayantilal Keshavji Chande ambaye ni mdau maarufu wa kundi la freemason hapa nchini aliusema alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha Clouds TV na Gerlad Ando,

    

Sir Chande alikuwa wazi sana na kukiri kwamba yeye ni mwanachama wa kundi la freemason ,na kwamba kundi lake yeye ni lile ambalo hukutana nchini kenya kwa mikutano yao.

Sir Chande akaendelea kwa kusema kwamba freemason sio uchawi wala haina uhusiano na mambo yoyote ya kishetani kinyume na inavyoongelewa na watu mbalimbali wengi wao ni wale ambao hawalijui kwa undani kundi hili ambalo. Kwa mujibu wa Bwana Chande ni kwa ajiri ya ushirikiano ,mshikamano na kusaidiana "If there is my company wants to offer a tender to other companies and if one of the companies is owned by a person who is a freemason then i will give the tender to the that person"alisema Chande akimaanisha kwamba kama kampuni kadhaa zinagombea tender na mmoja kati ya wenye makampuni ni wa freemason basi atampa tender hiyo mtu wa freemason  alisema hayo alipokuwa akisisitiza kwamba kwenye freemason hakuna faida za kifedha badala yake ni ushirikiano wa kawaida .

 

Bwana Chande anadai kwamba kipindi fulani  waliwahi kuhojiwa  kuhusu uhalali wa hekalu la freemason na kushukiwa kuwa walikuwa ni waabudu shetani (devil worshipers) ,"i took the journalists with the camera inside the freemason hall they pictured the hall then they said there is nothing bad and the government gave us permission to proceed with the freemaonry "Alisema Bwana Chande .

 

Chande aliongeza kwamba alama mbalimbali hutumika kama vielelezo katika kufundishia sheria na maadili ya freemasonry

 

Hata hivyo mahojiano hayo kati ya Chande na Gerald Ando wa Clouds TV yameonyesha utofauti mkubwa kati ya freemason tunayoisikia mitaani na ile iliyoelezwa na Bwana Chande .

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na habari nyingi kwenye vyombo vya habari kuhusu freemasonry ambapo picha mbalimbali za watu ambao aidha walikuwa wamesimama na Bwana Chande ama kwa namna moja au nyingine walionekana kama wameonyesha alama za freemason

Alama hii ya kipima pembe na Bikari hutumika na freemason katika mafunzo hasa ya kimaadili.

Katika Picha ni mkurugenzi wa makampuni ya IPP akiwa na Bwana Chande katika moja ya hafla hapa nchini Tanzania

Raisi mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Wiliam Mkapa akiwa katika moja ya hafla na Bwana Chande .

Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bwana Chande

Raisi wa awamu ya Pili Bwana Alli Hasan Mwinyi akiongea na Bwana Chande

 

Baadhi ya magazeti yalichapisha picha mbalimbali zinazounganisha freemason na ikulu

 

 

 

 

Post a Comment