Sunday, April 8, 2012

Athali za punyeto

ATHARI ZA KUJICHUA (MASTER BATION)

Tabia ya kujichua au kupiga punyeto ni kitu kilichozoeleka miongoni mwa vijana wengi kuanzia umri wa balehe ni hali ambayo imekuwa ya kawaida miongoni mwao. Hali hiyo siyo tu hutokea kwa vijana bali hata kwa watu wazima. Watu wanaofanya hivi hufanya kwa lengo la kujitosheleza wenyewe kimapenzi (self satisfaction). Watu hufanya kitendo hiki kwa malengo mbalimbali hasa wengi husema kwa lengo la kujiepusha na ngono, lakini je ni njia sahihi ya kuepusha ngono? Hili swali ambalo itabidi ujijibu mwenyewe baada ya kupata maelekezo yakina katika safu hii.

Zipo njia mbalimbali zinazotumika kujichua. Kwa mujibu wa utafiti wa hapa na pale, watu au wanaume wanaojichua hutumia sabuni, mafuta, wengine hujisugua sugua uume wanapokuwa wamelala lakini suala zima hapa ni kusugua uume kwa nguvu nakuvuta hisia na kuweka taswira ya kimapenzi ili kufikisha malengo yako.
Wapo watu wanaotumia midoli au vifaa maalum kwa shughuli hii, kwahiyo yapo makampuni katika baadhi ya nchi yanayotengeneza vifaa ambavyo hutumika kujichua au kupiga punyeto. Vifaa hivi ni uke uliotengenezwa bandia katika umbile la viungo vya siri ya mwanamke, ambavyo hutumiwa na mwanaume, vilevile vipo viungo vya kiume yaani uume bandia ambao hutumiaka na wanawake.

HALI INAYOJITOKEZA

Wakati mtu anapojichua hasa mwanaume, huvuta hisia na kutumia nguvu nyingi kusugua kichwa cha uume bila yeye mwenyewe kujijua. Kusugua kwa nguvu ndipo kunapoleta msisimko katika ubongo na kusababisha uume usimame na hisia zikiwa kali ndipo unkapofikia kilele. Hisia uvutwa kwa kufikiria taswira ya mwanamke yeyote na kuiweka karibu. Uume utasimama hadi kufikia kiwango cha juu na ndipo utakapoanza kutoa manii.
Hali hii ndiyo ilivyo hata kwa mwanamke. Watu wengine hasa kuvuta hisia inakuwa ngumu hiyvo hulazimika kuangalia picha za ngono au majarida ya ngono ndipo waweze kufanikisha malengo haya tofauti na kufanya ngono ya kawaida, kujichua kutumia nguvu nyingi katika kuvuta hisia za kimapenzi na kuhitaji uume usimame na ufikie kileleni. Hapa kila kitu ni cha kulazymisha, hata mfumo wa homoni unakuwa haupo tayari.

JINSI UUME UNAVYOSIMAMA
Katika hali yakawaida inayompelekea mwanaume afanye tendo la ndoa, kwanza kunakuwa na uamsho wa kawaida wa kimapenzi baada ya kumuona mwanamke, kisha mwili unajiandaa (Homornal changes). Mishipa ya damu mwilini inafunguka (vascular dilatations) yaani mishipa ya mwili mzima na ndiyo maana unapata msisimko, baada ya mishipa kufanguka au kutanuka, damu yote huishia chini kwa kasi na kwenda kujaa katika uume kwenye sehemu iitwayo ‘Urethral bulb’.
Damu inapojaa hapo ndipo inaposababisha uume usimame. Uume unasimama na kuendelea ambapo mzunguko wa damu hapo unakuwa mkubwa, damu inaenda na kurudi hadi tendo limapofikia katika kilele ambapo mishipa ya damu mwilini inapobana (vascular constriction) na damu kurudi katika hali ya kawaida na uume unalala. Kemikali inayosaidia zaidi hapa ni ile iitwayo ‘Nitric oxide’.vile vile majimaji (lubricant) au urethral mucus ambayo pamoja na kulainisha njia kwa ajili yakupitisha manii na uke ambapo hata mwanamke anapokuwa tayari kutoa .

MADHARA YA KUJICHUA
Tatizo hili ingawa hutumika kama njia ya kujizuia na tamaa ya ngono, kimsingi huwezi kufanya kitendo hiki bila kuzikaribisha tamaa hizi za ngono. Kwahiyo athari za tatizo hili tunaweza kuziweka katika makundi mawili, kwani athari za kisaikolojia na pili ni athari za kimwili.
Athari zakisaikolojia (Psychological effects) zinaanzia pale unapovuta hisia kazi za ngono. Bila kuwa na hisia kali huwezi kupata uamsho au ‘sexual avousal.’ Hisia kali ni za kulaizmisha kwahiyo zitakudumaza ambapo utashindwa msisimko wa kawaida hadi ufikiri sana.
Hali hii ikiendelea hata ukiwa na mwanamke utashindwa kusisimka haraka au utashindwa kubisha kufanya tendo kutokana na mgongano katika akili yako ambapo utajitahidi kuvuta hisia kali wakati mwanamke yupo hapo hapo karibu yako. Hapa ndipo utasikia mtu analalamika hapati hamu ya tendo la ndoa, akiwa na mwanamke uume huchelewa kusimama na hata ukisimama wakati wa tendo anawahi sana kumaliza na kushindwa kuendelea na tendo la pili.
Vilevile mtu wa aina hii huumwa na kichwa, kiuno na mgongo ingawa siyo mara kwa mara kwa wanawake wanaotumia viungo bandia vya uume nao huwa hawana hamu wala msisimko wowote wakiwa na wanaume.
Athari nyingine ni za kimwili (mechanical effects). Athari za kimwili ni maumivu ya uume kutokana na kusugua uume mara kwa mara, kulegea kwa misuli ya uume kutoana na kutumia nguvu kwa muda mrefu ili uweze kujitosheleza. Unaweza kupata michubuko katika uume au ndani ya njia ya mkojo. Unaweza kupata nagonjwa ya mishipa ya damu ya uume (microvascular effects) ambapo kutokana na kujisuguasugua mishipa inaweza kuziba hasa ile ya kurudisha damu nakufanya uume usimame bila kikomo kwa muda mrefu au usisimame kabisa.
Matatizo haya yote kwa pamoja husababisha upungufu mkubwa wa nguvu za kiume na kupoteza uwezo wa kufanya tendo la ndoa. Kwa ambao tayari wamekutwa na matatizo haya wataelewa vizuri. Hali hii ya kujichua hukufanya utumie hisia nyingi au nguvu nyingi na nishati nyingi kiasi cha nguvu zote zitumika kufikiri na kufanya kitendo.uelewe kwamba, ubongo unatumia asilimia 60 ya nishati yote mwilini na pia unapokojoa au kufikia mshindo mmoja, nishati au nguvu unaozotumia ni sawa sawa na mtu aliiyetembea kwa mguu umbali wa kilometa 15.
Kwa hiyo basi, kama wewe ni mwanafunzi na unaendekeza punyeto, ubongo wako utakuwa unachoka kila wakati kiasi kwamba utakuwa msahaurifu darasani, unakuwa unapoteza poteza kumbukumbu, mwili utakuwa mchovu na kila wakati utakuwa unasinzia daima hasa afya yako haitakuwa nzuri utakuwa mchovu daima.

USHAURI
Zipo njia nyingi za kuepuka tamaa za ngono siyo lazima ujichue au upige punyeto au ufanye masturbation (mastabesheni). Kitendo cha kujichua kinaashiria unaendekeza tamaa za ngono. Epuka vishawishi vya ngono kwa kutokusikiliza au kangalia vitendo hivyo kwa nia yoyote. Njia mojawapo ya kuepuka ngono au tamaa ya kujichua ni kushiriki mazoezi ya viungo na michezo ya kutumia akili kama draft, kuangalia michezo na kufanya miadala ya kielimu, vilevile kushiriki kikamilifu katika michezo.

4 comments:

Steve Finnell said...

you are invited to follow my blog

Anonymous said...

keep informing us Friday

Anonymous said...

sure watu wengi hawaelewi leo hta mimi nimeelewa hasa nitakapo msaidia mtu japo nilijua kidogo kuwa inamfanya mtu asiwe (active) katika mambo yanayohitaji akili (self esteem)Hongera bro

buy sizegenetics said...

Outstanding story there. What occurred after? Good luck!

http://173-203-100-146.static.cloud-ips.com/node/16139

http://smartmediamexico.com/micrositios/Megambrea/BBVA/everest/blogs/11/29/sizegenetics-system